Sunday, March 18, 2012

Furaha ya ngoma ingia ucheze



Mpiga ngoma akionyesha umahili wake wakati wa uzinduzi wa wiki ya Maji katika Mtaa wa Nyakanyasi Mjini Bukoba.habari zaidi gonga hapa...

Choo cha shimo,lazima uwe makini!



Hiki ni choo ninachotumiwa na wanafunzi wa hostel katika shule ya sekondari Mkombozi kata ya Katoma Manispaa ya Bukoba.Shule imefungwa na Serikali wiki hii kutokana na mazingira yasiyoridhsha kama haya.



habari zaidi gonga hapa...

Thursday, March 8, 2012

Usalama kwanza



Hapa ni barabara iendayo Kashai karibu na shule ya Msingi Tumaini mjini Bukoba.Utii wa sheria bila shuruti,somo bado halijakolea.

Friday, March 2, 2012

Uchafuzi wa mazingira

Gari likisomba uchafu kuupeleka eneo maalmu lililotengwa na Manispaa

Phinias Bashaya,Bukoba

Wakazi wa mji wa Bukoba wameonyesha hofu ya kulipuka kwa magonjwa ya kuambukiza kutokana na uchafuzi wa maji ya mto Kanoni yanayotumiwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya nyumbani.

Hofu hiyo imekuja kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha ambapo uchafu mwingi husombwa na maji ya mvua na kuingia katika mto huo unaopita katikati ya mji wa Bukoba.

Wakitoa malalamiko yao kwa nyakati tofauti,baadhi ya wananchi wa Kata za Bakoba ,na Hamugembe wamesema mto huo umejaa uchafu mwingia ambao unaweza kuhatarisha maisha yao kutokana na baadhi ya wananchi kutegemea maji yam to huo.

Mmoja wa wananchi hao Japhet Kyoma alisema hali mbaya ya uchafu inayoukabiri mto huo kwa kwa sasa inahatarisha maisha ya wananchi na kuwa na uwezekano mkubwa wa kutokea kwa magonjwa ya kuambukiza ikiwemo kipindupindu.

Pia mwananchi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Aisha Kamazima alidai uchafu mwingi unaozalishwa na wananchi wanaozunguka mto huo hurushwa ndani ya maji badala ya kuupeleka katika maeneo maalmu yaliyotengwa na Manispaa ya Bukoba.

Pia alisema wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi zilizopo karibu na mto Kanoni wako katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya kuambukizwa ambao kila mara huonekana wakichota maji katika mto huo kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya shuleni ikiwemo umwagiliaji wa maua.na usafi.

Aidha baadhi ya wananchi walilalamikia ujenzi holela unaoendelea kando yam to huo kuwa unachangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mto huku Manispaa ikilalamikiwa kwa kufumbia macho ujenzi unaoendelea.

Pia baadhi ya wananchi waliwataka viongozi wa Manispaa ya Bukoba kudhibiti hali hiyo inayoelekea kuhatarisha afya zao na kupendekeza kununuliwa kwa gari la kufyonza maji taka tofauti na ilivyo sasa.



Thursday, March 1, 2012

Enzi zile


Utamaduni wetu

Wednesday, December 22, 2010

albino aonyesha wasiwasi

"Nina wake watatu na watoto 19"

Sina imani na wakunga


Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa Kagera Burchard Mpaka ambaye ameonyesha wasi wasi wa watoto wanaozaliwa wakiwa albino kufia mikononi mwa wakunga.

Wednesday, December 15, 2010

Professa Tibaijuka

Furaha ya ngoma

mapokezi uwanja wa ndege

Ngoma maarufu ya 'akasimbo'kutoka wilayani Muleba ilipamba mapokezi ya Tibaijuka,ambaye ni Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mapokezi ya Prof Anna Tibaijuka leo Bukoba



Tuesday, December 14, 2010

Full Vipaji!



Wanafunzi wa shule ya sekondari Aman Boarding ya Mjini Bukoba wakionyesha umahili wao wa kuongoza bend wakati wa sherehe za kuwaaga kaka na dada zao.